The House of Favourite Newspapers

Efm radio yaunga mkono ujenzi wa shule

0

1Mkuu wa Vipindi wa 93.7 Efm, Dickson Ponela (kushoto) akipokea ramani ya madarasa kutoka kwa Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni, Rogers Shemwelekwa (kulia), Mhariri Mkuu wa Radio hiyo, Scholastica Mazula (katikati) wakiwa na wadau wengine.

2Mazula akifafanua jambo mbele ya Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni.3… akionesha ramani ya madarasa hayo.

KITUO cha Redio cha Efm 93.7 ambacho Makao Makuu yake yapo Kawe, jijini Dar jana kimeoneshwa eneo maalumu la kujenga madarasa wawili kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda za kuongeza idadi ya shule za kata katika wilaya hiyo ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi.

Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni, Rogers Shemwelekwa alimkabidhi Mkuu wa Vipindi wa Efm, Dickson Ponela ramani ya madarasa hayo sambamba na kumuoneshwa eneo la kiwanja kilichopo Kimara, jijini humo.

(Na Gabriel Ng’osha-GPL)

 

Leave A Reply