Home LOCAL ZAIDI YA MILIONI 60 ZATUMIKA KUTENGENEZA BARABARA ITUNDUMA

ZAIDI YA MILIONI 60 ZATUMIKA KUTENGENEZA BARABARA ITUNDUMA

Msimamizi wa miradi ya TASAF katika Kijiji cha Itunduma Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe Shabani Lukelema akizungumza kuhusu matengenezo ya  barabara yao katika kijiji cha Itunduma.

Msimamizi wa miradi ya TASAF katika Kijiji cha Itunduma Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe Shabani Lukelema akishiriki pamoja na wanufaika wa TASAF katika matengenezo ya  barabara yao katika kijiji cha Itunduma.

Wahariri wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya viongozi wa TASAF mkoani Njombe wakizungumza na wanufaika wa TASAF wanaotengeneza barabara ya kijiji cha Itunduma wakati walipotembelea mradi huo.

Mhariri wa EFM na ETV Scholastica Mazula akicheza na akina mama wanufaika wa TASAF waliopata ajira za mda katika mradi wa barabara ya kijiji cha Itunduma mara baada ya kutembelea mradi huio na kuzungumza nao.

Muonekano wa Kipande cha barabara iliyotengenezwa na wanufaika hao.

…………………………..

Mradi wa barabara wenye kilometa 4.4 unaounganisha Vijiji viwili vya Itunduma na Kichiwa vilivyopo Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe umetengenezwa kwa zaidi ya milioni 60 kupitia ajira za muda za wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa miradi ya TASAF katika Kijiji cha Itunduma Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe Shabani Lukelema, alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari ambao wako kwenye ziara yakukagua miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Amesema mradi huo ulianza Novemba 9, 2022 baada ya kuibuliwa na wananchi kwenye mkutano wao kutokana na barabara hiyo kutokuwa rafiki katika matumizi.

“Tunaishukuru sana Serikali kwakutuwezesha fedha kwaajili ya kutengeneza barabara hii,kwa sasa imekuwa rafiki na wananchi wananufaika nayo”, amesema Lukelema.

Kwa upande wake mkazi wa Kijiji cha Itunduma Mary Mfilinge amesema mradi huo umekuwa na manufaa makubwa kwao ikiwemo kupata ajira ambayo imesaidia kuboresha makazi yao pamoja na kununua mbolea.

“Ajira hii ilikuwani ya masaa manne ukimaliza unaenda kufanya kazi zako za nyumbani kwahiyo umetupa fursa nzuri za kijipatia kipato na kufanya shughuli zetu zingine za uzalishaji”, amesema

Nae Jesca Msigwa amesema awali barabara hiyo ilikuwa inawapa shida hususani kwa wanawake wanapoenda kujifungua kutokana gari kutopita kwa urahisi kurokana na ubovu wa barabara hata hivyo kwa sasa inapitik.

Mradi huu umetupa ajira ambayo kipato tunachokipata kimetusaidia kuendesha maisha yetu na familia zetu lakini pia kufanya shughuli ndogongogo za kiuchumi katika familia zetu jambo ambalo limeboresha maisha yetu kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na kipindi kilichopita.

Previous articleSOMA HABARI MAGAZETI YA LEO JUMATANO DISEMBA 27-2023
Next articleSOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DISEMBA 28-2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here