Bozi Boziana atembelea studio za Radio Times 100.5 Fm

November 22, 2010

Mwanamuziki mkongwe kutoka DRC Kongo, Bozi Boziana akijiandaa kwa mahojiano katika Kituo cha Times Radio F m 100.5 alipotembelea leo. Kutoka kulia ni Scholastica Mazula na Amina Singo watangazaji wa kituo hicho.
Mwanamuziki mkongwe kutoka DRC Kongo, Bozi Boziana akiwa na watangazaji wa Kituo cha Times Radio F m 100.5 Scholastica Mazula (kulia) na Amina Singo alipotembelea kituo hicho kilichopo Kawe Beach, Dar es Salaam leo. Boziana yupo nchini kwa mwaliko wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’

Mtangazaji wa kipindi cha mitikisiko ya pwani Khadija Shaibu maarufu kwa jina la Dida (wa pili kushoto) akiwa na wanenguaji wa Boziana Faila Boendi (kushoto) na Blausesse Ayembe (wa pili kulia) pamoja na mtangazaji wa kituo hicho Amina Singo.


chocolate princess boutique

November 22, 2010

...

Duka lenye vitu vya ukweli linalojulikana kwa jina la CHOCOLATE PRINCESS BOUTIQUE ambalo linapatikana pale Mikocheni kwa Mwalimu maeneo ya TALK OF THE TOWN limefungua blog mpya.

 

Jipatie vitu vya ukweli kwa bei nafuu kabisa kuanzia mavazi ya wakinadada pamoja na wakina kaka na watoto pia kwa kipindi hiki kinachokwenda kwenye sikukuu.

 

Tembelea blog ya duka hilo ili kujionea
vitu vinavyouzwa na uchague unachokipenda.
Wasiliana nao kwa simu namba:
+255 712 020272 / +255 773 787272
www.chocolateprincessboutique.blogspot.com