Waziri akimlisha Cake Meneja vipindi Scholastica Mazula huku akishuhudiwa na Mkurugenzi wa Sanaa BASATA Nd Omary Mayunga
Mh. Kapuya akimlisha keki kinara wa mitikisko ya pwani, mtangazaji Dida
Mwimbaji wa kundi la Coast Modern Taarab Omary Tego akiwatambulisha watangazaji wa Times 100.5 fm kutoka kushota ni Dj Kobo, Michael Saduka,Tego,Amani Missanah, Scholastica Mazula na Selemani Semunyu.
Taswira za matukio ya tamasha la mitikisiko ya Pwani 2009 ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa kazi ajira na maendeleo ya Vijana Mh Juma Kapuya na makundi tisa ya Taarab yaliyopo Jijini Dar yalitumbuiza makundi hayo ni pamoja na Jahazi, East African Melody, TOT, Five Star, Dar Modern, Coast Modern Taarab, Tandale na Supershine.

Tamasha hili ambalo lilifanyika katika viwanja vya Sabasaba (PTA)lilihudhuriwa na umati mkubwa wa watu kiasi cha kufanya Police kufunga milango saa 5 usiku huku mashabiki wengine wakirudi majumbani kwa kukosa kujirusha kwani ukumbi ulishajaa kiasi cha mashabiki 6000 walihudhuria tamasha hilo huku maelfu wengine walikosa





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivi jamani huu ushamba uliopitiliza tutauacha lini? Hii habari ya kulishana keki ovyo ovyo inaanza kuchosha sasa! Asili ya kulishana keki imetokea kwa wenzetu in the western world and it is usally reserved for the "bride and groom" to make their wedding day even more special. Hili tendo ni kwa ajili ya mume na mke au watu wenye uhusiano wa kimapenzi. Sio tabia nzuri kwa mwanamume yoyote kumlisha mwanamke yeyote tu keki! Inaonyesha kuwa hatelewi mambo na tunavamia-vamia tu mila za watu na ku-overdo things! Ni ushamba uliopitiliza na inadibi tuuache jamani especially kaka yetu Michuzi ana-post picha za madume mawili yanalishana keki! Kwanza kabisa habari ya Waziri kulisha keki watangazaji inahusu nini? Halafu cha kushekesha zaidi keki yenyewe ni ya mdoli! These types of cakes are really designed for little girls' birthdays, lakini sijui mshamba gani alitumwa kwenda kuoda hiyo keki akaichagua hiyo maana "ndio nzuri"! Tuulize jamani kabla hatujaanza kuvamia vamia mila na desturi ambazo hatujui zimeanzia wapi! Ni mambo ya aibu kwa kweli!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...